• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi atoa salamu kwa walimu katika siku ya walimu

    (GMT+08:00) 2020-09-09 19:18:59

    Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu kwa walimu na wafanyakazi katika sekta ya elimu katika nchi nzima, kabla ya kuadhimisha siku ya walimu nchini China inayoangukia tarehe 10 Septemba.

    Rais Xi amesema wakati wa mlipuko wa COVID-19, walimu katika nchi nzima walikabiliana na changamoto kwa ujasiri, kuendelea kufanya kazi na kutoa mchango muhimu katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona, kwa kujitolea kufundisha kwa njia ya mtandao wa Internet.

    Rais Xi pia amesema anatumai kuwa walimu watakumbuka kazi yao ya kuleta vipaji kwa ajili ya chama na taifa, kuendeleza mbinu za kufundisha kwa ajili ya zama mpya, na kutoa mchango zaidi katika kuwalea wajenzi na waendelezaji wa usoshalisti. China kwa sasa ina walimu milioni 17.32.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako