Takwimu zilizotolewa leo na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, mwezi Agosti, kiwango cha bei za bidhaa zinazotumiwa maishani (CPI) nchini China kiliongezeka kwa asilimia 2.4 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki, na kushuka kwa asilimia 0.3 ikilinganishwa na mwezi Julai.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa mwezi Agosti, kati ya aina nane kuu za bidhaa na huduma, bei za aina tatu ziliongezeka, moja ilikuwa sawa, na nyingine nne zilishuka ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |