• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serena Williams apata ushindi na kuingia hatua ya nusu fainali

    (GMT+08:00) 2020-09-10 15:46:17

    Serena Williams ameendelea kuonyesha kuwa, kuwa mama si kikwazo kwenye Tennis, na jana alionyesha umahiri wake tena na kufanikiwa kumshinda Tsvetana Pironkova na kufikia nusu fainali. Mwana mama huyo mwenye umri wa miaka 38 amefanikiwa kushinda mechi hiyo kwa kazi ngumu akianza kupoteza seti ya kwanza na hatimaye kushinda mbili zilizofuata …… 4-6, 6-3, 6-2, katika muda wa saa 2 na dk 12. Serena alifurahisha watu pale alipoonekana kumpungia mkono binti yake wakati akiendelea kucheza. Kwenye mechi nyingi kinda wa Japan Naomi Osaka leo anaingia uwanjani kutafuta bahati yake ya kucheza nusu fainali, na inawezekana kuwa akakumbana tena na Serena, na hapo itakuwa vigumu kujua nani ataibuka mshindi hasa ikizingatiwa kuwa kwenye mechi ya kwanza walipokutana Naomi Osaka aliibuka mshindi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako