• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanariadha wa Uganda Jacob Kiplimo awashangaza wapenzi wa riadha duniani.

    (GMT+08:00) 2020-09-10 15:46:43

    Jana usiku waganda waliendelea kutoa pongezi kwenye mitandao ya kijamii baada ya kijana mganda Jacob Kiplimo kupata ushindi kwenye mbio za meta 5000, kugombea ubingwa wa dunia na kumshinda bingwa mtetezi Selemon Barega wa Ethiopia kwenye mbio zilizofanyika huko Ostrava Jamhuri ya Czech. Jacob mwenye umri wa miaka 19 alitumia muda wa dakika 12: 48.63, mbele ya watazamaji 3,000 walioruhusiwa kuingia kwenye Uwanja wa Mestsky. Mara nyingi mbio za masafa ya kati huwa zinatawaliwa na wakimbiaji wa Ethiopia lakini safari hii, Jacob aliwaachana Selemon Barega na Lamecha Girma. Hata hivyo licha ya ushindi huo mzuri, Jacabo amefunikwa na rekodi ya mkenya Joshua Cheptegei aliyeweka rekodi ya dakika 12:46 kwenye mbio zilizofanyika huko Monaco. Katika miaka ya hivi karibuni Uganda imeanza kujitokeza kwenye mbio ndefu na kuleta ushindani mkubwa kwa magwiji wa Kenya na Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako