• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Eliud Kipchoge aelekea London na kuahidi kutetea taji la Marathon

    (GMT+08:00) 2020-09-10 15:47:06

    Mshikilia rekodi ya Dunia ya mbio za Marathon, Eliud Kipchoge wa Kenya ameahidi mbio za kuvutia, wakati akienda kutetea taji lake la London Marathon kwenye mbio zitakazofanyika Oktoba 4. Eliud amesema hana uhakika kama anakwenda kuweka rekodi ya dunia ambayo aliweka kwa muda wa saa mbili dakika 02 na sekunde 37, lakini amesema atajitahidi kupata ushindi katika mbio hizo. Hata hivyo amekuwa na malalamiko kiasi kuwa hali ya mazoezi haikuwa rahisi hasa kutokana na kuwa na vizuizi vya Covid-19. Amesema yeye na timu yake hawakuweza kufanya mazoezi katika hali ya kawaida katika kituo chao cha Kaptagat, hali ambayo ilipunguza uchangamfu kwenye maandalizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako