• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yanga yasema inafurahia uwezo wa wachezaji iliowasajili kwa msimu huu

    (GMT+08:00) 2020-09-10 15:47:25

    Klabu yaYanga imesema imejiridhisha na uwezo wa mastaa wao watano wapya wa kigeni na kusisitiza wakiimarika ndani ya siku 20 zijazo timu zitaumia. Mwenyekiti wa Yanga ambaye pia kitaaluma ni Kocha, Daktari wa falsafa, Mshindo Msolla amesema usajili wao msimu huu uko vizuri.

    Msolla alisema katika wachezaji wao watano wa kigeni hakuna mtu mwenye mashaka na vifaa hivyo kwani pesa zilizotumiwa na wadhamini wao GSM zimekwenda kihalali. Msolla amesema usajili wa safari hii ni mzuri tangu niingie ndani ya uongozi wa Yanga, na amaamini kuwa kikosi cha sasa kinaweza kurudisha heshima ya Yanga. Wachezaji waliosajiliwa msimu huu ni pamoja na washambuliaji Tuisila Kisinda, Yacouba Sogne, Michael Sarpong, viungo Mukoko Tonombe, Carlos Fernandez 'Carlinhos'. Kuhusu wachezaji wazawa waliosajiliwa alisema nao wamethibitisha ubora wao na kwa ambao hawakupata nafasi ya kuanza wanatakiwa kutambua hiyo ni hatua ya upana wa kikosi na wana

    nafasi ya kuzidisha mapambano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako