• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Aliyekuwa kiungo wa Simba ahamia Cs Constantine ya Algeria

    (GMT+08:00) 2020-09-10 15:47:44

    Mwanasoka kutoka Sudan aliyekuwa kiungo wa Simba, Sharaf Shiboub amejiunga na klabu ya Cs Constantine inayoshiriki Ligi kuu nchini Algeria kwa mkataba wa miaka miwili. Wakala wa Sharaf ametangaza kwenye ukurasa wake wa twitter kuwa Shiboub amejiunga na klabu hiyo yenye mtaji wa mashabiki katika ligi ya Algeria. Shiboub alisajiliwa na Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea katika klabu ya Al Hillal ya nyumbani kwao. Baada ya kumaliza mkataba, kiungo huyo hakuongezewa mkataba huku kukiwa na tetesi nyingi za mchezaji huyo kuhusishwa kutimkia Yanga. Mwishoni mwa msimu uliopita, Shiboub alikosa namba katika kikosi cha kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako