• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zanzibar-Wavuvi waiomba serikali kuwapatia vifaa vya kisasa vya uvuvi

  (GMT+08:00) 2020-09-10 18:34:14

  Wavuvi katika kijiji cha Chwaka kisiwani Zanzibar wameiomba serikali kuwapatia vifaa vya kisasa vya uvuvi wakisema kuwa vitasaidia kufikia uvuvi wa bahari kuu wenye tija zaidi katika kuwakomboa wananchi kiuchumi.

  Wakilalamikia kuwepo kwa vifaa visivyokidhi haja,wavuvi wa Chwaka wamesema iwapo watapatiwa nyenzo za kisasa wataweza kuvua maji makuu na kuwaacha samaki wadogo waweze kukua ili kuongeza mapambano ya uvuvi haramu.

  Wamesema ukilinganisha na hali ya sasa kiuchumi imekuwa vigumu kutokana na wingi wa wavuvi ukizingatia uchache wa vyombo unaleta msongamano katika harakati za uvuvi katika kukimu kimaisha.

  Aidha wameiomba serikali kuwapunguzia gharama za ukataji leseni za uvuvi hasa katika kipindi hiki kigumu kutokana na hali ya upepo kunachangia ukosefu wa samaki baharini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako