• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafafanua msimamo wake kuhusu miaka 75 tangu kuanzishwa kwa UM

    (GMT+08:00) 2020-09-10 21:14:01

    Wizara ya mambo ya nje ya China leo imetoa waraka wa msimamo wa China kuhusu miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, ambao umefafanua msimamo na mapendekezo yake kuhusu kazi ya Umoja huo, hali ya kimataifa, maendeleo endelevu, ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na COVID-19, na masuala mengine.

    Msemaji wa wizara hiyo Bw. Zhao Lijian amesema, waraka huo umeeleza kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kuichukulia miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa kama fursa muhimu ya kulinda kwa pamoja matokeo ya mafanikio ya vita dhidi ya Ufashisti, kupinga vitendo vya upande mmoja na umwamba, kuunga mkono kithabiti taratibu za pande nyingi, kulinda Katiba ya Umoja wa Mataifa, ili kulinda mfumo wa kimataifa wenye Umoja wa Mataifa kuwa kiini chake na utaratibu wa kimataifa ambao kiini chake ni sheria za kimataifa. Ameongeza kuwa China inapenda kushirikiana na nchi nyingine duniani kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako