• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa utalii wa Kenya apongeza mbio za London kuonyeshwa nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2020-09-11 16:15:37

    Wizara ya Utalii na Wanyamapori Kenya imepongeza hatua ya televisheni ya NTV kurusha moja kwa moja mashindano ya Marathon ya London mnamo Oktoba 4 kwenye majukwaa yake ya Kenya na Uganda, pamoja na yale ya kwenye mitandao ya kijamii. Waziri Balala amesema kwa sasa wakenya hawataweza kwenda kuwatazama na kuwaunga mkono wanariadha wake, na njia hiyo itawapa fursa kujionea wanariadha wao hodari wakishindana. Makala zilizopita za mashindano ya Marathon ziliweza kupokea wanariadha zaidi ya elfu 40, lakini safari hii ni wanariadha 70 tu hodari kutoka nchi mbalimbali duniani ndio wamealikwa kushiriki mbio hizo. Washiriki wakenya ambao mara nyingi huvutia wapinzani wengi, safari hii wanafursa nzuri ya kuitanganza Kenya duniani. Wakenya Eliud Kipchoge na Brigid Kosgei walishinda Mashindano ya Marathon ya wanaume na wanawake ya 2019, safari hii watakuwa na wakenya wenzao, Ruth Chepng'etich na Vivian Cheruiyot.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako