• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Abdillahie Yussuf wa Tanzania apelekwa tena Wales kwa mkopo

    (GMT+08:00) 2020-09-11 16:16:16

    Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Abdillahie Yussuf amejiunga na Wrexham ya Wales inayocheza Ligi Daraja la Tano England, maarufu kama National League kwa mkopo wa hadi mwisho wa msimu kutoka Blackpool FC ya Daraja la Tatu. Wrexham inakuwa timu ya tatu kwa Adi Yussuf kupelekwa kwa mkopo tangu asajiliwe Blackpool FC Mei mwaka jana kwa mkataba wa miaka miwili – baada ya awali kupelewa klabu yake ya zamani, Solihull Moors na Boreham Wood msimu uliopita. Yussuf alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichoshiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Juni mwaka jana nchini Misri. Alitua Blackpool baada ya kufunga mabao 21 katika mashindano yote Solihull Moors, yakiwemo mawili dhidi ya Seasiders kwenye mchezo wa marudiano wa Raundi ya Pili ya Kombe la FA na kuiwezesha timu hiyo kumaliza nafasi ya pili kwenye National League. Mchezaji huyo wa zamani wa akademi ya Leicester City, rekodi yake nzuri zaidi ya msimu ni kufunga mabao 29 katika mechi 39 akiwa na Oxford City msimu wa 2014- 2015 baada ya awali kuchezea Burton Albion, Mansfield Town na Crawley Town.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako