• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Victor Wanyama alifunga bao la kwanza la Montreal Impact

    (GMT+08:00) 2020-09-11 16:16:33

    Mwanasoka wa Kenya Victor Wanyama hatimaye amefungua ukurasa wake wa ufungaji wa magoli kwenye timu yake ya Montreal Impact miezi kadhaa baada ya kuhamia kwenye Soka la Ligi Kuu Canada. Kiungo huyo alifunga bao lake kwenye mechi iliyochezwa jana, goli alilofunga katika dakika ya 53 dhidi ya wapinzani wao Toronto FC. Pablo Biatti alikuwa ameifungia Toronto FC bao katika dakika ya 32 kabla ya Wanyama kusawazisha kipindi cha pili. Bao la nyota huyo wa Kenya hata hivyo halikutosha kuwaokoa Montreal kutokana na kushindwa kumdhibiti Jozy Altidore aliyeongeza bao la pili. Wanyama ambaye alianza kusota Uingereza akiwa na Tottenham, aliamua kuhamia Canada ambao mpaka sasa amekuwa na wakati mgumu kuonyesha makali yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako