• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UHURU AZIMA PENSHENI KWA WABUNGE WA ZAMANI

  (GMT+08:00) 2020-09-11 18:10:39

  Matumaini ya wabunge wa zamani waliohudumu kati ya miaka ya 1984 na 2001 ya kufurahia pensheni ya Sh100,000 kila mmoja kila mwezi, sasa yamezimwa baada ya Rais Uhuru Kenyatta kukataa kutia saini mswada uliopendekeza walipwe pesa hizo.

  Hiyo jana, Rais Kenyatta aliurejesha bungeni mswada huo na maelezo ya kuwataka wabunge waondoe kipengele kinachopendekeza pensheni hiyo akisema "haiwezekani kisheria".

  Alisema pensheni hiyo itagharimu mlipa ushuru Sh450 milioni kila mwaka, na itachochea makundi mengine ya wafanyakazi wa umma kuitisha nyongeza ya malipo hayo ya kustaafu ambayo serikali haiwezi kumudu.

  Mswada huo wa marekebisho ya sheria ya pensheni ya wabunge ulidhaminiwa na Kiongozi wa Wachache John Mbadi na ukapitishwa na wabunge mnamo Agosti 5, 2020, kisha ukawasilishwa kwa Rais Kenyatta.

  Ulipendekeza kuwa jumla ya wabunge 290 waliostaafu kati ya 1984 na 2001 walipwe Sh100,000 kila mwezi kuanzia Julai 1, 2010. Hii ilimaanisha kuwa kila mmoja wao angepokea malimbikizo ya karibu Sh11 milioni endapo Rais angetia saini mswada huo. Wakenya wengi walikuwa wameghadhabishwa na mswadahuo ambao waliutaja kuwa kejeli kwa uchumi wa taifa haswa wakati huu mgumu ambapo janga la covid-19 limelemaza sekta nyingi za uchumi wa taifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako