• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TWCC yazindua tuzo za wanawake wajasiriamali

  (GMT+08:00) 2020-09-11 18:11:07

  Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), kimezindua tuzo za wanawake waliofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2020 katika sekta za viwanda na biashara zenye lengo la kutambua na kuheshimu wanawake waliofanikiwa na wale wanaochipukia katika sekta za viwanda na biashara.

  Tuzo hizo zilizinduliwa Jumatano wiki hii, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama hicho, Jacquiline Maleko ambapo amesema kuwa tuzo hizo zinalenga kuonyesha mchango wa mwanamke mjasiriamali katika kukuza uchumi wa nchi na kuchochea maendeleo ya jamii.

  Akizungumza katika uzinduzi huo Jacquiline mesema wanawake ni nguzo muhimu sana katika maendeleo ya jamii yoyote na kwamba wana uwezo wa kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya viwanda na biashara endapo wataaminiwa na kupewa nafasi yakufanya hivyo.

  Jacquiline ameongeza kuwa zoezi la kusajili washiriki wa tuzo litaendelea kwa kipindi cha mwezi mmoja na litafungwa Oktoba 9 mwaka huu na kwamba sherehe za utoaji wa tuzo kwa washindi zinatarajiwa kufanyika Novemba 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

  Amesema utoaji wa tuzo hizo utaambatana na uzinduzi wa Jarida la Wanawake 100 Wajasiriamali waliothubutu kitachotumika kutangaza kazi mbalimbali za wanawake wajasiriamali nchini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako