• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na India zafikia makubaliano ya kupunguza mvutano mpakani

    (GMT+08:00) 2020-09-11 18:42:47

    Waziri wa mambo ya nje wa China na mwenzake wa India Bw. Jaishankar wamefikia makubaliano yenye sehemu tano kuhusu maendeleo ya hali kwenye mpaka wa nchi zao na kuhusu ushirikiano kati ya pande mbili.

    Taarifa imesema mawaziri hao wamekubaliana kuwa pande mbili zinatakiwa kufuata makubaliano yaliyofikiwa kati ya viongozi wa nchi hizo mbili kuhusu kuendeleza uhusiano kati ya nchi zao, na kutoruhusu tofauti kati yao kuwa migogoro. Taarifa pia imesema hali ya sasa ya mpakani haina maslahi kwa upande wowote, na kukubaliana kuwa majeshi ya nchi hizo mbili mpakani yaendelee na mazungumzo, yaache makabiliano na kuweka umbali kati yao ili kupunguza mivutano.

    Mawaziri hao wamesema hali itakapotulia, pande mbili zinatakiwa kuharakisha kazi ya kujenga upya hali ya kuaminiana na kuleta amani na utulivu mpakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako