• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani isivunje mfumo wa kimataifa wa kudhibiti silaha

    (GMT+08:00) 2020-09-11 19:58:13

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema, Marekani inapaswa kusimamisha mara moja kitendo cha kuvunja mfumo wa kimataifa wa makubaliano ya kudhibiti silaha, kinachoweza kuharibu utulivu wa kimkakati duniani.

    Mwanahabari mmoja wa Marekani kwenye kitabu chake kipya amesema, rais Donald Trump wa nchi hiyo alidokeza kuwa Marekani inaendeleza silaha mpya za nyuklia. Baadhi ya wanasiasa wa nchi hiyo wamekiri habari hiyo.

    Bw. Zhao amesema Marekani ikiwa nchi yenye nguvu zaidi ya silaha za nyuklia, si kama tu imekataa kutekeleza jukumu la kupunguza silaha hizo, bali pia inachochea ushindani kati ya nchi kubwa, na kuimarisha zaidi ujenzi wa uwezo wa silaha za nyuklia kwa nguvu kubwa, na inatakiwa kutoa maelezo kwa jumuiya ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako