• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya ulinzi ya China yazungumzia ripoti ya Marekani kuhusu maendeleo ya jeshi na usalama wa China kwa mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2020-09-14 09:05:44

    Msemaji wa wizara ya ulinzi ya China Bw. Wu Qian jana alitoa maelezo kuhusu ripoti iliyotolewa na wizara ya ulinzi ya Marekani kuhusu maendeleo ya jeshi na usalama wa China kwa mwaka 2020, akisema huu ni ushahidi wa Marekani kuipaka matope China na jeshi lake.

    Bw. Wu Qian amesema huu ni mwaka wa 20 tangu Marekani ianze kutoa ripoti hiyo, ambacho ni kitendo cha umwamba na uchokozi kinachoharibu uhusiano kati ya majeshi ya nchi hizo mbili, na China inaipinga kithabiti ripoti hiyo.

    Bw. Wu Qian amesisitiza kuwa China inashikilia kujiendeleza kwa njia ya amani, kutekeleza sera ya ulinzi yenye mtazamo wa kujilinda na mkakati wa kijeshi unaozingatia kuimarisha ulinzi wa taifa. Amesema maendeleo ya jeshi la China yanalingana na mahitaji ya kulinda mamlaka ya taifa, maslahi ya usalama na maendeleo, China hailengi nchi yoyote na wala haitishii nchi yoyote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako