• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Serikali Yasaka Sh100 Bilioni Kufufua Biashara

  (GMT+08:00) 2020-09-14 16:52:06

  Serikali inalenga kupata angalau Sh100 bilioni za kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo.

  Alhamisi iliyopita, serikali ilitangaza kubuni hazina ya kutoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo hasa walioathiriwa na makali ya janga la corona.

  Katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanywa wiki jana katika Ikulu ya Nairobi, serikali iliamua kuweka kitita cha Sh10 bilioni kwenye hazina hiyo.

  Jumla ya Sh5 bilioni zitawekwa katika kipindi cha fedha cha mwaka huu, huku Sh5 bilioni nyingine zikiongezwa katika mwaka wa fedha wa 2021/2022, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu.

  Mkutano huo ulioongozwa na Rais Uhuru Kenyatta ulihudhuriwa pia na Naibu Rais William Ruto.

  Serikali ilisema inatarajia hazina hiyo itapokea fedha zaidi kutoka kwa mashirika ya kifedha yanayojihusisha na masuala ya ustawishaji wa maendeleo, na mabenki ya kibinafsi lengo likiwa ni kufikisha Sh100 bilioni. Maelfu ya wafanyabiashara kote nchini walipata pigo tangu janga la corona lilipothibitishwa nchini mnamo Machi, hadi wengi wao wakalazimika kufunga biashara zao.

  Hali hii ilichochewa sana na kanuni kali zilizotolewa nchini na ulimwenguni kote katika juhudi za kuepusha ueneaji wa maambukizi ya virusi vya corona.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako