• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Bolt yazindua huduma mpya ya usafiri kwa bei nafuu

  (GMT+08:00) 2020-09-14 16:52:31

  Kampuni ya utoaji huduma ya usafiri barani Ulaya na Afrika (BOLT), imezindua huduma mpya, nafuu ya usafiri inayofahamika kwa jina la 'Bolt Lite'.

  Huduma hiyo ambayo inalenga kuwapatia abiria huduma bora za usafiri kwa bei nafuu, itapatikana katika mikoa Arusha, Mwanza na Dodoma.

  Akizungumzia ujio wa huduma hiyo mpya ya usafiri, Meneja wa Bolt nchini Tanzania, Remmy Eseka alisema huduma ya 'Bolt Lite' inalenga kufanya huduma za usafiri katika maeneo ya mijini kupatikana kwa bei nafuu zaidi ili wateja wao wafaidike na huduma za Bolt.

  Alisema pia lengo ni kuongeza idadi ya safari na mapato kwa madereva ambao ndio washirika wakubwa wa Bolt. Aidha, alifafanua kuwa Bolt Lite ni huduma ya hiari kwa madereva wa Bolt ambayo inawaruhusu kusimamia mapato yao wakati wanakubaliana malipo na wateja wao ili kuendana na hali halisi ya janga la maambukizi ya Virusi vya COVID-19. Alisema Bolt ina watumiaji zaidi ya milioni 30 katika nchi zaidi ya 35 barani Ulaya na Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako