• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TENNIS: Naomi Osaka anyakua taji La US Open

  (GMT+08:00) 2020-09-14 17:16:58

  Naomi Osaka alidhihirisha ubabe wake katika mchezo wa tenisi kwa kujinyanyua taji la mashindano ya tennis ya US Open kwa kumshinda mpinzani wake Victoria Azarenka katika nchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki. Ushindi huo ulimpa Osaka ambaye ni raia wa Japan taji lake la tatu la Grand Slam na la pili kwenye mashindano ya US Open. Osaka alizidiwa maarifa katika seti ya kwanza na akajipata chini ya pointi 3-0 mwanzoni mwa seti ya pili. Hata hivyo, alijinyanyua na kutawala raundi 10 kati ya 12 zilizofuatia. Hiyo ilikuwa fainali ya kwanza kwa Azarenka, 31, kushiriki tangu 2013. Nyota huyo raia wa Belarus alishindwa kudhibiti ukali wa mipakuo ya Osaka aliyemvurumishia fataki nzito nzito kuanzia mwanzo wa seti mbili za mwisho.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako