• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Olunga afunga bao licha ya timu yake kufungwa 2-1 na Tosu katika Ligi Kuu ya Japan

  (GMT+08:00) 2020-09-14 17:17:17

  Mshambuliaji wa Harambee Stars ya Kenya Michael Olunga ambaye anachezea timu ya Kashiwa Reysol ya Japan alifunga bao la kufutia machozi wakati timu yake ilipofungwa bao 2 – 1 na Sagan Tosu katika mechi ya Ligi Kuu ya Japan iliyochewa hapo jana. Olinga kwa sasa anaongoza jedwali la wafungaji bora wa Ligi hiyo kwa magoli 16 kutokana na mechi 15. Bao lake dhidi ya Tosu lilipatikana katika dakika ya 24. Ushawishi wa Olunga unazidi katika kambi ya Reysol tangu aongoze kikosi hicho kupanda ngazi na kufikia Ligi Kuu mwishoni mwa msimu uliopita. Katika mchuano wa mwisho ulioshuhudia Reysol wakiwapiga Gamba Osaka 3-0 ligini, Olunga alipachika wavuni bao la kwanza katika dakika ya pili na kufikisha jumla ya magoli 15 kapuni mwake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako