• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kuimarika kwa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Umoja wa Ulaya kutongeza imani kwa uchumi wa dunia wakati wa COVID-19

  (GMT+08:00) 2020-09-14 18:41:09

  Wakati mkutano wa viongozi wa China, Ujerumani, na Umoja wa Ulaya utakaofanyika kwa njiaya video unapokaribia, wataalamu na wasomi wengi wa China na nchi za nje wamesema, yakiwa makundi makubwa mawili muhimu ya kiuchumi duniani, kuimarishwa kwa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Umoja wa Ulaya kutaongeza imani na uhai katika uchumi wa dunia wakati wa janga la COVID-19. --- ana maelezo zaidiā€¦

  Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 45 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Umoja wa Ulaya. Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti wa Ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda iliyo chini ya Wizara ya Biashara ya China Bw. Zhang Jianping ameeleza kuwa, hii itatoa ishara muhimu kwa dunia kuwa China na Ulaya zinaimarisha mawasiliano na ushirikiano, ili kulinda utaratibu wa pande nyingi, na biashara huria. Anasema:

  "Kutokana na janga la virusi vya Corona duniani, uchumi wa dunia umedorora. Kwa wakati huu, mazungumzo kati ya China na Ulaya yatachangia katika kuhimiza mchakato wa utandawazi wa dunia na ushirikiano wa kiuchumi wa kanda hii, kulinda utulivu wa mnyororo wa usambazaji wa bidhaa duniani na mnyororo wa thamani duniani, na kuleta mustakabali mzuri zaidi kwa soko la dunia, vilevile yatanufaisha makampuni ya pande hizo mbili na pande nyingine zinazohusika."

  Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Idara Kuu ya Forodha ya China, kati ya mwezi Januari hadi Agosti mwaka huu, thamani ya biashara kati ya China na Umoja wa Ulaya, ambao ni mwenzi mkubwa wa pili wa biashara wa China, ilifikia RMB yuan trilioni 2.81, sawa na dola za kimarekani bilioni 411, ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.4, na kuchukua asilimia 14 ya thamani ya jumla ya biashara ya kimataifa. Mwenyekiti wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Umoja wa ULaya nchini China Bw. Joerg Wuttke anasema:

  "Tunatumai kufungua mlango au kufanya ushirikiano. Hivi sasa makubaliano ya uwekezaji kati ya China na Ulaya yanatarajiwa kufikiwa. Tunatumai kuwa China na Umoja wa Ulaya zitaweza kupata ufumbuzi ndani ya wiki kadhaa zijazo, na kufikia maafikiano. Wakati uchumi wa dunia unaposhuka, tunahitaji vitu vinavyosaidia, na Ulaya na China zina uwezo wa kujenga hali kama hii."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako