• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapendekeza kuondoa vizuizi vya uuzaji wa chakula nje

  (GMT+08:00) 2020-09-14 19:21:38

  Waziri wa kilimo na vijiji wa China Bw. Han Changfu amehudhuria mkutano wa mawaziri wa kilimo na uhifadhi wa maji wa kundi la nchi 20 (G20), ambapo ametoa pendekezo la kuondoa vizuizi vya uuzaji wa chakula na bidhaa muhimu za kilimo.

  Bw. Han amesema, hivi sasa maambukizi ya virusi vya Corona yameenea kote duniani, mnyororo wa biashara ya chakula na mnyororo wa ugavi wa chakula duniani umeathiriwa vibaya, hivyo kundi la hilo linapaswa kushirikiana kulinda usalama wa chakula na utulivu wa kilimo duniani.

  Ametoa mapendekezo matatu, ambayo ni kushirikiana kuinua uwezo wa uzalishaji wa chakula, kuimarisha ushirikiano wa uwekezaji na biashara wa kilimo duniani, na mwisho, kuhimiza kupunguza taka zinazotokana na chakula.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako