• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China awasiliana na viongozi wa Ujerumani na Umoja wa Ulaya kwa njia ya mtandao

  (GMT+08:00) 2020-09-15 09:06:04

  Rais Xi Jinping wa China amesema China na nchi za Ulaya zinapaswa kuhimiza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kuendelea vizuri na kwa utulivu, na kuchangia juhudi za kimataifa za kupambana na janga la COVID-19, kufufua uchumi na kulinda haki.

  Rais Xi amesema hayo alipowasiliana na Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel ambaye pia ni mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Ulaya, mwenyekiti wa Baraza la Ulaya Bw. Charles Michel na mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Ulaya Bibi Ursula von der Leyen kwa njia ya mtandao. Amesisitiza kuwa pande hizo mbili zinapaswa kushikilia mambo manne, ambayo ni kuishi pamoja kwa amani, kufungua mlango na kushirikiana, kushikilia taratibu za pande nyingi, na kutatua masuala kwa njia ya mazungumzo.

  Viongozi wa Ulaya wamesema China ni mwenzi muhimu wa kimkakati wa kuheshimika wa nchi za Ulaya, na hivi sasa dunia inahitaji pande hizo mbili kuimarisha mshikamano na ushirikiano, na kulinda kwa pamoja taratibu za pande nyingi, ili kukabiliana vizuri na changamoto mbalimbali za kimataifa

  Kwenye mkutano huo, pande hizo mbili zimetangaza kusaini makubaliano muhumu kati ya China na Umoja wa Ulaya, kuharakisha mazungumzo kuhusu Makubaliano ya Uwekezaji, na kuanzisha mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu suala la mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako