• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Kiyeng ameshinda Chepkoech kwa mara ya kwanza

    (GMT+08:00) 2020-09-15 16:08:36

    Mshindi wa nishani ya fedha katika Olimpiki za Rio 2016, Hyvin Kiyeng, alimpiku bingwa wa dunia, Beatrice Chepkoech kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu. Hii ni baada ya Kiyeng kuibuka malkia wa mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji kwenye kivumbi cha ISTAF Berlin, Ujerumani zilizofanyika Jumapili. Wakenya hao wawili walikuwa unyo kwa unyo hadi kiunzi cha mwisho. Hata hivyo, Kiyeng aliyeibuka bingwa wa dunia mnamo 2015, alimpigia hesabu Chepkoech katika hatua ya mwisho na kufika utepeni kwa muda bora wa dakika 9:06.04. Kiyeng alimbwaga Chepkoech kwa mara ya mwisho mnamo 2017 walipotifua kivumbi cha Doha Diamond League. Miaka mitatu baadaye, mtimkaji huyo aliridhika na medali ya fedha katika mbio za World Athletics Tour zilizoandaliwa jijini Berlin, Ujerumani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako