• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • BASKETBALL: Ulinzi Warriors wasajili wanavikapu wawili

  (GMT+08:00) 2020-09-15 16:08:56

  Mabingwa wa kitaifa wa mchezo wa vikapu nchini Kenya, Ulinzi Warriors, wamejinasia huduma za wachezaji wawili kwa minajili ya kampeni za msimu ujao katika Ligi Kuu ya Shirikisho la Vikapu la Kenya (KBF). Meneja wa timu hiyo, Stephen Bartilol, amethibitisha kwamba Brans Nzioka na Gideon Ndambuki ndio wanavikapu wapya ambao wamesajiliwa na Warriors kutoka Laiser Hill Academy. Mbali na maazimio ya kuhifadhi ubingwa wao wa kitaifa wa KBF, Warriors wanapania pia kutamba kwenye Michezo ya Majeshi barani Afrika mwakani na katika Ligi ya Vikapu barani Afrika (BAL) itakayoanza Januari 2021.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako