• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Azam FC yatamba kuendeleza kipigo

  (GMT+08:00) 2020-09-15 16:09:34

  Baada ya ushindi katika michezo miwili mfululizo waliopata timu ya Azam FC, uongozi wa timu hiyo umetamba kuendeleza ushindi katika michezo inayofuata ya ligi kuu. Azam FC katika michezo miwili iliyocheza ya ligi hiyo, imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania, kisha wakashinda 2-0 dhidi ya Coastal Union, michezo yote ilifanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamanzi jijini Dar. Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Azam FC, Thabit Zakaria amesema, wanashukuru kuanza Ligi vizuri kwa kupata pointi zote sita muhimu huku akisema kuwa kilichobaki kwao ni kuendeleza ushindi katika michezo inayofuata.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako