• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ukuaji wa uchumi wa China warejeshwa kwa hatua madhubuti katika mwezi Agosti

  (GMT+08:00) 2020-09-15 19:02:25
  Idara ya takwimu ya China imesema, viashiria muhimu vya uchumi vimeendelea kurejeshwa katika mwezi Agosti, huku msukumo na uhai wa maendeleo ukizidi kuongezeka, na ukuaji wa uchumi unarejeshwa kwa utulivu.

  Hata hivyo, Msemaji wa Idara hiyo Bw. Fu Linghui amesema, viashiria vingi viko chini kuliko mwaka jana wakati kama huo, na uendeshaji wa uchumi bado unakabiliwa na changamoto nyingi. Ameongeza kuwa uchumi wa dunia unakabiliwa na changamoto kubwa kufufuka, haswa kutokana na kuwa maambukizi ya virusi vya Corona hayajazuiliwa kwa hatua zenye ufanisi, na sintofahamu ni kubwa. Katika kipindi kijacho China itaendelea kutekeleza vizuri hatua za kuhimiza uchumi kurejeshwa kwa hatua madhubuti.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako