• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kiwanda Cha Mananasi Kujengwa Gatundu Kaskazini

  (GMT+08:00) 2020-09-15 19:18:46

  SERIKALI ya Kaunti ya Kiambu ina mpango wa kujenga kiwanda cha mananasi katika eneo la Gatundu Kaskazini.

  Gavana wa Kiambu Dkt James Nyoro alisema kuna haja ya kujenga kiwanda hicho kwa sababu wakazi wengi eneo hilo wanapanda minanasi kwa ajili ya kuzalisha mananasi.

  Kiwanda hiki kinatarajiwa kuwafaidi pakubwa kiuchumi, na pia vijana wengi watanufaika na kupata ajira.

  Aidha amesema katika muda wa miezi mitatu ijayo kaunti hiyo ya Kiambu itafanya utafiti ili kubainisha eneo bora la kujuenga kiwanda cha mananasi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako