• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kufungwa kwa muda mrefu kwa baa na vilabu vya usiku kumelazimisha Hazina kupunguza makadirio yake ya ushuru kwa Sh45.8 bilioni

  (GMT+08:00) 2020-09-15 19:20:47

  Kufungwa kwa muda mrefu kwa baa na vilabu vya usiku kumelazimisha Hazina kupunguza makadirio yake ya ushuru kwa Sh45.8 bilioni, na kuipatia serikali ukusanyaji mpya wa mapato miezi mitatu tangu kuanza kwa mwaka wa fedha.

  Waziri wa fedha Ukur Yatani amepunguza matarajio ya ushuru ambayo mengi yanatokana na uuzaji wa pombe na sigara hadi Sh195.6 bilioni kutoka Sh241.4 bilioni zilizowekwa mnamo Juni licha ya kuongezeka kwa ushuru kutoka Oktoba 1.

  Hazina ufungwaji wa baa kutokana na Corona kumenyima serikali mapato ambayo yanatokana na uuzaji wa vinywaji na sigara ambazo uchangia asilimia 75 ukusanyaji wa ushuru.

  Uuzaji wa pombe umeshuka kusababisha kampuni kama East Africa Breweries Limited (EABL) kutangaza kushuka kwa asilimia 39 ya faida yake na kufikia Sh7 bilioni kwa mwaka ulioishia Juni 2020.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako