• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China asema China itashikilia kufungua mlango zaidi

    (GMT+08:00) 2020-09-16 09:25:49

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesema uchumi wa China umeungana kwa kina na uchumi wa dunia, China haiwezi kupata maendeleo kwa kujitenga na dunia, na maendeleo ya dunia pia yanahitaji China, na bila kujali mabadiliko ya mazingira ya nje, China itashikilia kithabiti kufungua mlango zaidi.

    Bw. Li amesema hayo akihutubia mazungumzo maalumu ya wanaviwanda kwenye Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF). Amesema janga la COVID-19 limeleta changamoto mpya kwa uchumi wa dunia ambao tayari ulikuwa na matatizo mengi, haswa biashara ya kimataifa. Kwa hiyo inapaswa kulinda kwa pamoja mchakato wa kurahisisha biashara na uwekezaji, na kurejesha mnyororo wa kimataifa wa uzalishaji na ugavi wa bidhaa na mawasiliano ya watu, ili kufufua uchumi wa dunia.

    Amesema uchumi wa China unadumisha mwelekeo wa kufufuka kwa utulivu, na kama hakuna mabadiliko makubwa China itatimiza malengo yake makuu ya maendeleo, na uchumi wake utaendelea kukua mwaka huu, hata hivyo, uchumi wa China unakabiliwa na matishio na changamoto zinazohitaji kuondolewa.

    Aidha, Bw. Li amesema janga la COVID-19 limeleta changamoto kubwa kwa uchumi wa dunia, ambao mchakato wa kufufuka kwake unakabiliwa na sintofahamu na utachukua muda mrefu, jumuiya ya kimataifa inapaswa kujitahidi kustawisha tena uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako