• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FAO yasema janga la COVID-19 limefanya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya 2030 kuwa mgumu

    (GMT+08:00) 2020-09-16 09:28:59

    Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetoa ripoti likisema juhudi za dunia kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 ziko nyuma, na janga la COVID-19 limesababisha hali hiyo kuwa ngumu zaidi.

    Mwaka 2015 Umoja wa Mataifa uliyataja malengo 17 ya maendeleo endelevu kuwa mpango wa kutimiza siku za baadaye endelevu. Lakini kutokana na ripoti ya ufuatiliaji wa maendeleo ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu kwa mwaka 2020, janga la COVID-19 limeleta changamoto zaidi katika kutimiza malengo hayo.

    Mtaalamu wa uchumi wa shirika hilo Bw. Maximo Torero, amesema nchi mbalimbali duniani zimekumbwa na mabadiliko kutokana na janga hilo, na zinatakiwa kuchukua hatua mwafaka ili kutimiza malengo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako