• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Yoshihide Suga achaguliwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Japan

  (GMT+08:00) 2020-09-16 16:08:54

  Bunge la Japan limemteua kiongozi mpya wa chama tawala nchini humo LDP, Yoshihide Suga kuwa waziri mkuu mpya, akichukua nafasi ya Sinzo Abe.

  Suga alichaguliwa na mabunge yote mawili, akishinda kwa kura 314 katika baraza la chini la bunge lenye wajumbe 465, na kwa kura 142 katika baraza la juu la bunge lenye wajumbe 245.

  Waziri mkuu huyo mpya anatrajiwa kuunda baraza jipya la mawaziri, wengi wakiwa mawaziri waliofanya kazi chini ya Shinzo Abe.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako