• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mke wa rais wa China ahutubia Maadhimisho ya miaka 25 ya Mkutano wa Wanawake Duniani uliofanyika mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2020-09-16 16:56:46

    Mke wa China, Bibi Peng Liyuan amesisitiza kuwa China siku zote ni mtetezi na mhimizaji wa mambo ya wanawake na kutokomeza umaskini duniani.

    Bibi Peng amesema hayo alipohutubia kwa njia ya video katika maadhimisho ya miaka 25 ya Mkutano wa Wanawake Duniani uliofanyika mjini Beijing, ukiwa na kaulimbiu ya "Jukumu la binadamu la kutokomeza umaskini katika karne ya 21 na umuhimu wa wanawake". Amesema mwaka huu China itatimiza lengo la kutokomeza umaskini vijijini, ambao ni mchango muhimu kwa mambo ya maendeleo ya binadamu. Amesisitiza kuwa katika hatua hiyo, wanawake wengi wa China wameitikia wito wa serikali wa kupunguza umaskini na kuonesha umuhimu mkubwa.

    Bibi Peng pia ametoa wito kwa nchi mbalimbali kutoa elimu bora yenye usawa kwa wanawake, kuhakikisha wanawake wanapewa huduma za kimsingi za afya, kuondoa unyanyasaji na upendeleo kwa wanawake, ili kuwawezesha wanawake wote kuishi maisha mazuri, na kufanya juhudi katika kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako