• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya watumiaji wa mtandao wa 5G nchini China yapita milioni 110

    (GMT+08:00) 2020-09-16 17:08:31

    Mkuu wa taasisi ya utafiti wa mawasiliano ya simu na upashanaji wa habari ya China Bw. Liu Duo amesema, hivi sasa, idadi ya watumiaji wa mtandao wa 5G nchini China imepita milioni 110, na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu, idadi ya vituo vya mtandao wa 5G itapita laki 6 na kufikia miji yote nchini China.

    Bw. Liu pia amesema, mpaka kufikia mwaka 2025, makampuni ya mawasiliano ya mtandao ya China yanatarajia kupata uwekezaji wa dola za kimarekani bilioni 251.26. Pia matumizi ya kibiashara ya mtandao wa 5G yataingiza dola za Marekani bilioni 266.04 za matumizi ya mtandao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako