• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • MBIO ZA MAGARI: Barabara za Kenya zahitaji ujasiri, wasema madereva wa kimataifa

  (GMT+08:00) 2020-09-16 17:17:57

  Madereva wa kimataifa wanasubiri kwa hamu kubwa kushiriki mbio za magari za Safari Rally zitakazorejea kwenye ratiba ya Shirikisho la Mbio za Magari Duniani (WRC) mwaka 2021. Madereva hao walisema barabara za Kenya zinazohitaji ujasiri mkubwa pamoja na wanyama pori ni vitu vinavyowapa hamu zaidi ya kwenda Kenya kwa mashindano hayo yaliyofanyika mara ya mwisho mwaka 2002. Mbio hizo zilipangwa kurejea mwaka huu, lakini zikaahirishwa hadi 2021 kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona. WRC imethibitisha kuweka Safari Rally kwenye ratiba ya kwanza ya 2021 ili kuwafahamisha madereva mashindano yatakayofanyika msimu ujao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako