• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Onyango alenga kurejea KPL kwa kishindo

  (GMT+08:00) 2020-09-16 17:18:21

  Stephen Onyango aliibuka wa pili katika orodha ya wafungaji bora wa Ligi ya Kitaifa ya Supa nchini Kenya (NSL) katika msimu wa mwaka 2019-20, na anatazamia kupata timu ya kuchezea katika Ligi Kuu ya Kenya (KPL) katika msimu ujao wa 2020-21. Onyango alisalia bila klabu kuanzia mwezi Aprili baada ya kisa cha kwanza cha virusi vya Corona kuripotiwa nchini humo. Fowadi huyo matata alitemwa na wanabenki wa KCB Januari na akarejea kambini mwa Fortune Sacco waliowapiku Nairobi City Stars na Nairobi Stima katika vita vya kuwania saini yake. Hata hivyo, kipindi chake katika kikosi cha Fortune Sacco katika Kaunti ya Kirinyaga kilikuwa kifupi baada ya michezo kusitishwa nchini Kenya kutokana na janga la Corona mwezi Aprili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako