• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Barabara za maeneo yenye kipato cha chini kukarabatiwa Kenya

  (GMT+08:00) 2020-09-16 18:42:02

  Serikali ya Kenya imetoa shilingi bilioni 5.8 za kukarabati zaidi ya kilomita 400 za barabara kwenye makaazi yenye mapato ya chini, katika mji mkuu Nairobi.

  Mradi huo unatarajiwa kuanza kabla ya mwisho wa mwezi huu na utasimamiwa na Mamlaka ya Barabara za mijini nchini humo (Kura).

  Mkurugenzi Mkuu wa Kura (DG) Silas Kinoti amesema kazi zinaanza wiki ijayo.

  Waziri wa uchukuzi James Macharia, amesema uboreshaji wa barabara hizo ni moja ya hatua zinazochukuliwa kurahisisha usafiri kwenye maeneo yanayolengwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako