• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China ampongeza Yoshihide Suga kwa kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Japan

  (GMT+08:00) 2020-09-16 18:48:43

  Rais Xi Jinping wa China leo ametoa salamu za pongezi kwa Bw. Yoshihide Suga kwa kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Japan.

  Kwenye salamu hizo, rais Xi ameeleza kuwa China na Japan ni marafiki wa karibu na majirani wema, pia ni nchi muhimu barani Asia na duniani kwa ujumla. Amesema kukuza uhusiano wa muda mrefu, wenye urafiki na ushirikiano kati ya pande hizo mbili, kunalingana na maslahi ya kimsingi ya wananchi wa pande hizo mbili, vilevile kunachangia amani, utulivu na ustawi wa Asia na dunia. Pia amesisitiza kuwa pande hizo mbili zinatakiwa kufuata kanuni na makubaliano yaliyofikiwa, kuhimiza ujenzi wa uhusiano unaoendana na matakwa ya zama mpya, na kuzinufaisha nchi hizo mbili na wananchi wao, ili kuchangia katika kulinda amani ya dunia na kuhimiza maendeleo ya pamoja.

  Naye waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang pia amempongeza Bw. Yoshihide Suga kwa kuteuliwa kuwa waziri mkuu, na kusema anatumaini kuwa China itashirikiana na Japan kuimarisha mawasiliano ya kirafiki na ushirikiano wenye ufanisi katika sekta mbalimbali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako