• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baadhi ya nchi wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa waiunga mkono China kuhusu suala la Hong Kong na la Xinjiang

  (GMT+08:00) 2020-09-16 19:03:35

  Baadhi ya wajumbe wa nchi wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa wametoa kauli ya kuiunga mkono China katika suala la Hongkong na la Xinjiang.

  Hayo yamejiri katika mjadala wa kawaida wa mkutano wa 45 wa Baraza hilo, ambapo mjumbe kutoka Burundi amesema, Burundi inaipongeza China kwa kutunga sheria ya kulinda usalama wa taifa ya Mkoa wa Utawala Maalumu wa Hong Kong. Amesema sheria hiyo inasaidia kuhakikisha sera ya "nchi moja, mifumo miwili", inahimiza ustawi na utulivu wa muda mrefu wa Hong Kong, na inasaidia kuhakikisha haki za kibinadamu za watu wa Hong Kong. Burundi pia inaipongeza China kwa kupambana na ugaidi na watu wenye itikadi kali mkoani Xinjiang, na inaona kuwa hatua husika zimeondoa kihalisi vyanzo vya ugaidi.

  Naye mjumbe wa Ethiopia amesema, mambo ya Hong Kong ni mambo ya ndani ya China, na Ethiopia inaunga mkono kithabiti sera ya China ya "nchi moja, mifumo mwili", inapinga baadhi ya nchi kulifanya suala la haki za binadamu liwe la kisiasa, na kuingilia kati mambo ya ndani ya China kwa kutumia suala la Hong Kong.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako