• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mazingira mapya ya kupambana na COVID-19 yawasubiri wanafunzi wa Kenya wakati shule zikijiandaa kufunguliwa

  (GMT+08:00) 2020-09-16 19:20:19

  Wanafunzi, walimu na wafanyakazi katika mashule nchini Kenya watatakiwa kuvaa barakoa muda wote, kudumisha umbali wa kijamii, na kupima dalili za virusi vya Corona kila siku mara shule zitakapofunguliwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.

  Hatua hizo ziko katika mwongozo wa usalama uliotolewa na wizara ya elimu kuongoza ufunguaji wa shule ambazo zilifungwa Machi 15 kufuatia mlipuko wa janga la virusi vya Corona.

  Mwongozo huo umetoa hatua zitakazohakikisha usalama wa wanafunzi, kuzuia, kugundua mapema na kudhibiti virusi vya Corona katika taasisi za elimu.

  Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Elimu imesema, wahusika wa kutoa chakula na kufanya usafi katika taasisi hizo watatakiwa kuwa na vifaa binafsi vya kujikinga ili kuboresha afya ya msingi na usafi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako