• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ECOWAS yaitaka Mali kuunda serikali inayoongozwa na raia ili kuondolewa vikwazo

    (GMT+08:00) 2020-09-16 19:20:59

    Jumuiya ya Uchumi wa Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) imewataka viongozi wa kijeshi nchini Mali kuunda serikali ya mpito ya kiraia ili kuondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya nchi hiyo.

    Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa ECOWAS ambaye ni rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo alipokuwa akiongea na wanahabari baada ya mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika Magharibi kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Mali. Amesema hali ya Mali inahitaji suluhisho la haraka la kuunda serikali ambayo itaanza mchakato wa kuleta utulivu nchini humo.

    Rais Akufo-Addo ameongeza kuwa, ingawa mkutano huo haukufikia makubaliano yoyote, msimamo wa ECOWAS wa kuundwa kwa serikali ya mpito ya kiraia bado haujabadilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako