• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: New Generation yaiadabisha Green Queens mabao 15-0

  (GMT+08:00) 2020-09-17 16:05:55

  Timu ya soka ya New Generation imeanza vyema Ligi Kuu ya Soka la Wanawake Zanzibar kwa ushindi mnono wa mabao 15-0 dhidi ya Green Queens katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa kwenye uwanja Mao Zedong. New Generation yenye maskani yake Kwahani walijipatia mabao yao kupitia Zamoyonce James na Warda Abdulhakim ambao walifunga mabao matatu kila mmoja, huku Hawa Faraham, Hafidha Juma na Maimuna Khamis wakifunga mabao mawili mawili, na Hawa Ali Juma, Riziki Abubakar na Mwajuma Abdalla wakafunga bao moja kila mmoja. Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena Jumamosi ya Septemba 19 mwaka huu, kwa mchezo mmoja ambao utawakutanisha Jumbi Queens na Kidimni, ambao utachezwa kwenye uwanja wa Mao Zedong saa 10:00 za jioni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako