• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Aubameyang kuendelea kuichezea Arsenal

  (GMT+08:00) 2020-09-17 16:08:26

  Hatimaye nahodha na mshambuliaji wa Arsenal, Pierre Emerick Aubameyang amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake makuu Kaskazini mwa jijini London. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Gabon amesaini mkataba mpya, baada ya kukamilisha mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo, ambao ulionyesha kila sababu ya kutaka kuendelea kufanya kazi na nyota huyo aliyesajiliwa mwaka 2018, akitokea Borussia Dortmund chini ya Arsene Wenger. Aubameyang mwenye umri wa miaka 31 ataendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal hadi mwaka 2023, baada ya kusaini dili hilo ambalo litamfanya awe analipwa mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako