• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa waraka kuhusu uhakikisho wa ajira mkoani Xinjiang

    (GMT+08:00) 2020-09-17 18:20:41

    Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China leo imetoa waraka kuhusu uhakikisho wa upatikanaji wa ajira katika mkoa wa Xinjiang.

    Waraka huo unasema, Xinjiang imechukua kuhimiza ajira kuwa mradi mkubwa wa wananchi, na kuendelea kuongeza nguvu za kutoa mafunzo ya ajira, kupanua njia za kupata ajira, kuongeza nafasi za ajira. Hatua hizo zimefanya hali ya ajira kuwa na mwelekeo mzuri, na kipato cha watu wa makabila mbalimbali mkoani humo kimeongezeka.

    Wakara huo pia unaonyesha kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, sera na mfumo wa uhakikisho wa kazi na ajira mkoani Xinjiang zimekamilika zaidi, nafasi za ajira zimeongezeka, miundo ya ajira imeboreshwa zaidi, sifa ya nguvukazi imeinuka kidhahiri, na mapato ya wakazi na wafanyakazi yameongezeka kwa madhubuti.

    Waraka huo pia umesisitiza kuwa, Xinjiang inahakikisha haki za kimsingi za wafanyakazi kwa mujibu wa sheria, kutunga na kutekeleza sheria na kanuni mbalimbali za mkoa huo, kuhakikisha haki za wafanyakazi kupata ajira kwa usawa, usalama wa kazi, uhuru wa kuabudu na matumizi ya lugha na maandishi ya kikabila.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako