• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda-Suubula.com yashirikiana na Longhorn kuuza vitabu mtandaoni

    (GMT+08:00) 2020-09-17 19:53:01
    Jukwaa la uuzaji bidhaa mtandaoni la Uganda la Suubula.com limeshirikiana na kampuni ya uchapishaji ya Longhorn Uganda kuwezesha umma kununua vitabu vya watoto mtandaoni.

    Hivi sasa,wazazi wanalazimika kwenda umbali mrefu kufikia maduka ya vitabu ili kuchagua vitabu kwa ajili ya watoto wao,na mara nyingi baadhi ya vitabu haviwekwi katika rafu kwa sababu ya ukosefu wa nafasi.

    Hali hii inaonekana kubadilika huku kampuni ya Longhorn Publishgers Uganda ikisaini mkataba na soko la mtandaoni linalokua kwa kasi nchini Uganda la Suubula.com,ili kuuza vitabu mtandaoni.

    Afisa Mkuu Mtendaji wa Suubula.com,Camble Hope amesema kinachohitajika ni mtu kuingia kwenye mtandao wa Suubula.com na kutafuta vitabu vya Longhorn.Alisema hapo mtu atapata mamia ya vitabu vya elimu vyenye ubora vya kuwasaidia na kuwaongoza watoto katika elimu yao yote.

    Aliongeza kuwa baada ya hapo unafanya malipo kama ulivyoongozwa katika mtandao wa Suubula.com halafu vitabu hivyo vitawasilishwa nyumbani au kazini kwako ndani ya kipindi cha masaa 24.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako