• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Askari 23 na wanamgambo 31 wauawa katika mapigano nchini Afghanistan

    (GMT+08:00) 2020-09-18 09:17:49

    Serikali ya mkoa wa Nangarhar nchini Afghanistan imethibitisha kuwa askari 23 na wanamgambo 31 wameuawa, na wengine kadhaa walijeruhiwa katika mapigano yaliyotokea kwenye mkoa wa Nangarhar na mkoa wa Badghis usiku wa Jumatano, wakati juhudi za kutimiza amani zikiendelea.

    Msemaji wa mkoa wa Nangarhar amewaambia waandishi wa habari kuwa kikosi cha usalama kilijibu mashambulizi ya wanamgambo kwenye wilaya za Khogiani, Shirzad na Hesaraka, na askari 20 na wanamgambo 29 waliuawa na askari wengine 15 na wanamgambo 20 walijeruhiwa.

    Katika mkoa wa Badghis magharibi, kikosi cha usalama kilipambana na washambuliaji waliovamia ofisi za wilaya ya Qadis, ambapo askari 3 na wanamgambo wawili waliuawa.

    Mapigano hayo yalitokea wakati mazungumzo ya amani kati ya ujumbe wa serikali na wawakilishi wa Taliban yanaendelea huko Doha nchini Qatar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako