• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa kuongeza uwezo wa kukabiliana na ugaidi na itikadi kali

    (GMT+08:00) 2020-09-18 09:19:19

    Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuhimiza taratibu za pande nyingi na ushirikiano wa kimataifa, na kuongeza uwezo wa kukabiliana na ugaidi na itikadi kali ili kukuza na kulinda haki za binadamu.

    Hayo yamesemwa na kiongozi wa ujumbe wa China katika Umoja wa Mataifa huko Geneva Bw. Chen Xu kwenye semina juu ya mapambano dhidi ya ugaidi na itikadi kali. Amesisitiza jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, na kutoa wito wa utekelezaji thabiti wa mkakati wa Umoja wa Mataifa katika kupambana na ugaidi.

    Amesema mkoa unaojiendesha wa kabila la Wauyghur wa Xinjiang wa China ulikuwa ukisumbuliwa na ugaidi, ufarakanishaji na itikadi kali ya kidini, magaidi walifanya maelfu ya mashambulizi ya kigaidi, na kutishia sana maisha ya watu na utulivu wa kijamii.

    Kutokana na kutekeleza hatua mbalimbali za kukabiliana na ugaidi na kuondoa umaskini kwa mujibu wa sheria, China imepata mafanikio makubwa katika kuzuia ugaidi na kulinda haki za binadamu za makabila yote, na katika miaka minne iliyopita, hakuna tukio hata moja la shambulizi la kigaidi mkoani humo. Ameongeza kuwa hatua hizo zimetoa mchango muhimu na uzoefu mzuri kwa juhudi za kimataifa za kupambana na ugaidi na itikadi kali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako