• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa waraka kuhusu miaka 30 tangu China ijiunge na operesheni za kulinda amani za UM

  (GMT+08:00) 2020-09-18 10:46:23

  Ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China leo imetoa waraka kuhusu miaka 30 tangu China kujiunga na operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.

  Waraka huo unasema China imekuwa nguvu kuu ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani duniani, na hadi sasa wanajeshi wa kulinda amani wa China wameshiriki kwenye operesheni za kulinda amani katika zaidi ya nchi 20 zikiwemo Cambodia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Liberia, Sudan, Lebanon, Sudan Kusini, Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati, na kutoa mchango muhimu katika kuhimiza utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani, kulinda usalama na utulivu wa kikanda, na kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi hizo.

  Waraka huo unasema ikiwa mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, China itaendelea kuunga mkono operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.

   

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako