• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Gor Mahia kuendelea kubeba taji la Ligi Kuu baada ya SDT kufuta kesi iliyofunguliwa na KPL

  (GMT+08:00) 2020-09-18 16:32:29

  Jopo la Usuluhishi wa Migogoro ya Michezo nchini Kenya (SDT) limetupilia mbali kesi iliyowasilishwa na kampuni ya KPL inayoendesha Ligi Kuu ya Kenya, ikipinga maamuzi ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) kumaliza michezo ya Ligi Kuu ya msimu wa 2019-20 na kutawaza Gor Mahia mabingwa. Katika maamuzi yake, Mwenyekiti wa SDT John Ohaga alisema kwamba Afisa Mkuu wa KPL Jack Oguda hakutafuta njia nyingine za kutafuta suluhu kati ya KPL na FKF kabla ya kushtaki shirikisho kwa SDT. Ohaga pia aliamua kwamba Oguda, ambaye alikuwa mlalamishi katika kesi hiyo, aliwasilisha mashtaka bila ya kuwa na idhini kutoka kwa vikosi vya Ligi Kuu ya soka ya humu nchini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako